GALLERY

KAZI MWANZONI

Kwa sasa Lindi Jumbo inashugulika na ujenzi wa awali wa maeneo ya mgodi kwa minajiri ya kuandalia barabara na madaraja kwa ajili ya ujenzi utakaofuata. Mtazamo wa hatua kwa hatua unalenga kusaidia kuelimisha jamii ya hapo na kuwaelekeza wajenzi, taratibu nzuri, uthibiti wa ubora na usalama wa mazingira ya kazi.

MAENDELEO YA MIUNDO MBINU KATIKA WILAYA

Maendeleo ya matarajio ya hali ya juu kuhusu amana ya madini ya kinywe katika Wilaya ya Ruangwa imevuta makampuni binafsi ya ujenzi na wizara za serikali kuwekeza na kuendeleza Wilaya katika ujenzi wa mgodi wa madini ya kinywe wa Lindi Jumbo.