LINDI JUMBO LTD ni kampuni ya Kitanzania iliyosajiliwa kutafiti na kuchimba madini. Kwa sasa tunaendeleza mgodi wa madini ya kinywe (graphite) wa Lindi Jumbo uliopo katika Mkoa wa Lindi kwenye ukanda wa kusini mwa Tanzania. Utafiti sahihi usio shaka umeisha kamilika na mazungumzo ya mapatano yanaendelea ili kupata mshiriki wa kimkakati wa kuharakisha maendeleo ili mradi uweze kuanza uzalishaji mapema mwaka 2020.
Tunajivunia kusema kwamba hii inaifanya kampuni ya LINDI JUMBO LTD kuongoza na kuwa ya KWANZA kuwa na mgodi unaozalisha kinywe chini ya Utawala Mpya wa Tanzania.
TAMKO LA MISHENI
Falsafa ya kampuni ni kutafiti, kuendeleza na kuchimba madini kwa gharama ya chini mahali tulipo na tukiajiri tulipo. Uzoefu wetu umetufundisha neno moja muhimu; nalo ni kudumisha mahusiano na mawasiliano imara kati yetu na jamii inayotuzunguka). Kipimo cha mawasiliano ndicho daima kimekuwa kielelezo cha hali yetu. Nchini Tanzania kuna msemo wa Kiswahili usemao, “tupo pamoja” ambao unatoa taswira nzuri ya yatarajiwayo na mradi wa Lindi Jumbo. Huu ndio msimamo wa kampuni, kufanya kazi na jamii inayowazunguka na kuruhusu hisia ya jamii kujisikia kuwa tuko nao katika kila hatua.
SAFARI YETU YA MIAKA SITA
Ilianza kwa unyenyekevu uliotupeleka kuwa kiongozi wa kuendeleza kinywe.
2016 ⇒
-
- Kulenga ubora wa hali ya juu
Hatua ya pili ya uchorongaji wa kutumia aina hiyohiyo ya kuchoronga miamba(RC drilling) ulijikita kwenye eneo lenye ubora wa daraja la juu la madini ya kinywe uliopo upande wa magharibi mwa hifadhi ya Gilbert arc. Hii ilifanyika kwa kusudi la kuongeza imani katika maeneo yaliyotarajiwa kuwa na madini.
2018 ⇒
-
- Kuboresha vyanzo vya madini
Hatua ya tatu ya kuchoronga na kuchimba mitaro(trenches) ilikamilika na kusababisha rasilimali kuongezeka kimataifa toka tani milioni 29.6 hadi 41.8 – ongezeko la asilimia 41.3%. Hii iliwezekana kwa kufanikisha uchorongaji na uchimbaji mitaro wa jumla ya mita 5,000 kwa wakati ule.
2015 ⇒
-
- Kazi ya mwanzo ya kuchoronga.
Mpango wa kuchoronga kwa kutumia mashine ya kuchorongea yenye kutoa vipande vidogovidogo vya miamba kwa kwa kutumia kifaa maalum cha kukatia miamba (RC drilling) na chenye ncha ya almasi ulifanywa kwa kutumia kampuni ya kuchoronga ya Kitanzania ambayo ilitoa taarifa muhimu za mwanzo zihusuzo madini ya kinywe.(data za nguvu za mwanzo ya kinywe).
2020
UZALISHAJ
KUANZA KARIBUNI !!!!