SUSTAINABILITY

Falsafa

Falsafa ni kuvumbua, kuendeleza na kuchimba amana ya madini ya nishati wakati tukiwa hapo tulipo na kuajiri watu wa hapo hapo.

Kwa uzoefu wa Lindi Jumbo ilioupata, kila mara kumekuwa na jambo moja muhimu ambalo limetufanya kuimarisha uhusiano na mawasiliano na jamii. Njia ya mawasiliano daima imekuwa kipimo cha hali ya uhusiano. Kwa kujumuisha wanavijiji na bodi za vijiji katika kila hatua ya mradi, sio tu kwa kuajiri vibarua na kuchangia katika matukio ya kijamii bali hata kujenga mazingira ya kuwa pamoja. Nchini Tanzania kuna msemo usemao kwa Kiswahili, “tupo pamoja” ambao unatoa mwangwi/(taswira) mzuri kuhusu mradi wa Lindi Jumbo. Huu ni mfano ambao kampuni imechukua kufanya kazi na wenyeji na kuruhusu wajisikie kuwa nasi.

Kwa mda mrefu, Mkataba wa makubaliano na mkataba wa Hakuna mikataba ya migogoro, iliwekewa sahihi kati ya kampuni, vijiji na Wilaya. Mikataba hii imepokelewa kwa mikono miwili na kuibua hisia ya kujenga msingi wa yatayofuata. Hadi sasa mikataba yote imeheshimiwa.

MICHANGO YA KIJAMAA

Kwa upande wa michango ya kijamaa, kampuni hujishugulisha na mabaraza ya vijiji na ofisi ya Wilaya ili kuelewa msaada unapohitajika. Kila ombi hutazamwa na Bodi ya Wakurugenzi na kampuni hutoa msaada kama inawezekana. Katika kila ombi la kuchangia, kudhamini, kutoa ruzuku au matukio ya nia njema, Lindi Jumbo imekuwa ikifuatia kwa miezi au hata baada ya miaka au muda kuona maendeleo yaliyofanyika na kuona mafanikio yaliyofikiwa kwa kila suala husika. Kampuni inapenda kukwepa kutoa fedha  bila kufuatilia matokeo au kuona fedha yake ikitumiwa vibaya.

Yafutayo ni machache ambayo Lindi Jumbo imehusika na inaona fahari kujumuika nayo:-

USALAMA

Tunafuata kanuni nzuri kabisa za viwango vya usalama kutoa mazingira yaliyo salama na imara wakati wote kwa wafanyakazi wetu, wakandarasi na wanajumuia. Uangalifu zaidi na wa ziada unatekelezwa wakati wafanyakazi wetu na wale wa wakandarasi wanapofanya kazi za uchimbaji madini.